Klabu ya Ngara Stars ya mjini Ngara jana October 05,2014,imeonesha mwanzo mzuri katika ushiriki wake wa Ligi soka Ngazu ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera, inayotarajiwa kuanza kesho kutwa Jumatano Octoba 08,2014 ,baada ya kuifunga Kabanga FC katika mchezo wa Ngao ya Hisani unaoashiria kuanza kwa michuano ya Ligi hiyo.


Mgeni rasmi ambae ni Kaimu Mkurugenzi wilaya ya Ngara mkoani Kagera Helman Hume (kushoto) akifatilia mchezo huo katika uwanja wa kokoto..Katika Hotuba yake aliiagiza idara ya Michezo wilaya kuweka mkakati wa kukutana na wadau wa michezo wilayani humo ili kuangalia namna ya kuufanyia maboresho uwanja wa Kokoto.pembeni yake ni Godfrey Brayan mwakalishi wa Vilabu kutoka Chama cha soka wilaya-NDFA.



Katika mchezo huo uliochezwa jana jioni uwanja wa Kokoto mjini Ngara, Timu hizo zilitoka sare ya kufungana goli 1-1 katika Dakika 90 na mwamuzi kuamuru ipigwe mikwaju ya penalty ili kumpata mshindi.

Katika hatua hiyo timu zote zilipiga Penati 6 ambapo Kabanga FC ilikosa penati 2 na kupata 4 huku Ngara Stars ikikosa 1 na kupata 5 na hivyo kushinda kwa jumla ya magoli 6 - 5.





Mashabiki na Wapenzi wa Ngara Stars wakifurahia baada ya timu yao kubeba Ngao ya Hisani waliyokabidhiwa na Mgeni rasmi ambae ni Kaimu Mkurugenzi wilaya ya Ngara Helman Hume.

Ligi ya wilaya ya Ngara ianatarajiwa kuanza Jumatano Octoba 08,2014, kwa timu 8 shiriki kugawanywa katika vituo vitatu, ambavyo ni Rulenge, Ngara mjini na Benaco.

Timu hizo ni:-

Kabanga FC

Rulenge White Stars

Mabawe FC

Ngara Stars

Ngara Boys FC

Walimu FC

Rusumo FC 

Na Benaco Stars.
 
Top