Baadhi ya wagombea wamezungumzia changamoto walizokutana nazo katika kampeni za uchaguzi huku wapiga kura nao wakionyesha ari kubwa ya kutaka kushiriki kuwachagua viongozi wao.
Ikiwa ni siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi serikali za mitaa nchini kote afisa mtendaji wa kata ya Goba manispaa ya kinondoni jijini Dar es salaam Bw. Salum Mzaganya amenusurika kipigo baada ya kuruhusu ratiba za vyama vya CHADEMA na CCM kufanya mikutano sehemu moja huku akitaka chama kimoja wapo kijiondoe chenyewe.
Hali hiyo ilisababisha kikosi cha polisi wilaya kawe chini ya mkuu wa upelelezi wilaya Afande Mgonja kufika eneo la tukio kuingilia kati na kutoa ushauri wa vyama vyote kuhamisha mikutano yao kwenda zaidi ya mita mia moja kutoka eneo la awali CCM wakihamisha makao kuelekea mbezi ya kimara wakati chadema wakiamriwa kuelekea tangi bovu.
Wakizungumzia hali hiyo viongozi na makada wa vyama vya CCM na CHADEMA baada ya kukubali ushauri wa kuhamisha mikutano yao pamoja na kulalamikia kuwathiri kisiasa wameeleza udhaifu wa afisa mtendaji huyo huku kila chama kikishutumu.
CREDIT: MALUNDE1