Wagombea wa uenyekiti wa vitongoji kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (ccm) katika kijiji cha Nyakiziba kata Murukulazo ya wilayani ngara mkoani kagera waliokuwa wamepita bila kupingwa baada ya wagombea wa chadema kuwekewa pingamizi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika jana siku ya jumapili ya tarehe 14/12/2014 wamejiudhuru kwa kile walichosema kuwa hawako tayari kuongoza wakati hawajachaguliwa na wananchi. Akiongea mmoja wa viongozi waliojiudhuru Bwana Ibunga John amesema sababu kuu iliyopelekea walio kuchukua uamuzi huo ni kwamba hawawezi kuongoza watu ambao hawakuwachagua na zaidi wamedai hali hiyo ya kupita bila kupingwa ingewasababishia kukosa ushirikiano na wana jamii wanaoishi nao.

Wananchi wa Nyakiziba wamesema kwa hali ilivyokuwa wasingesirikiana na viongozi hao katika jambo lolote huku baadhi yao wakidai kuwa wasingewatambua viongozi hao waliokuwa wamepita bila kupingwa maana wamenyima haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi bila sababu za msingi.

Akiongea diwani wa kata hiyo Bwana Mkiza Vyamungu amesema kuwa vifaa vya kupiga kura havikupelekwa kijijini hapo kwa sababu tayari wagombea wa ccm walikuwa wamepita bila kupigwa baada ya wagombea wa chadema kuwekewa pingamizi hivyo hakukuwa na haja ya uchaguzi.



 
Top