Uchaguzi wa serikali za mitaa nchini uliofanyika jana umeendelea kumwaga damu ambapo mwanamme aitwaye Simeo Isaka (42),mkazi wa kijiji cha Ngokolo kata ya Bukomela wilayani Kahama mkoani Shinyanga, ameuawa kwa kukatwa na jembe kichwani na watu wasiojulikana wakati akishangilia ushindi wa mgombea wa Chadema ngazi ya mwenyekiti wa kijiji.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Na Kadama Malunde-Shinyanga.