Baadhi ya viongozi wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wamepata mwaliko wa kuhudhuria Bunge la ulaya nchini Ubelgiji, na kukutana na viongozi wa bunge hilo, pamoja na kuhudhuria mkutano Mkuu wa 27 wa chama cha CDU nchini Ujerumani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kaimu katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalim amesema, ujumbe huo wa CHADEMA utafanya mazungumzo na viongozi wa bunge hilo, juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea hapa nchini.

Amesema kama chama kikuu cha upinzani, watakaowakilisha ni ujumbe wa viongozi wakuu wa Chadema na wamejipanga kufanya mazungumzo, maalumu kwa mustakabali wa taifa la Tanzania.

Aidha mwalimu amesema wakiwa nchini ujerumani viongozi hao watazungumzia changamoto mbalimbali zinazolikabili taifa

Ujumbe huo wa CHADEMA tayari umeshaanza safari yake, na utakuwa kwenye ziara hiyo kwa muda wa siku kumi.

 
Top