Serikali imetengua uteuzi wa Wakurugenzi sita wa Halmashauri, na kuwasimamisha kazi wengine watano kupisha uchunguzi, kutokana na kubainika kuchangia kuvurugika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, uliofanyika tarehe 14, mwezi huu.
Akitangaza hatua hiyo kufuatia ripoti iliyoibua madudu yaliyofanyika katika uchaguzi huo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Hawa Ghasia amesema uamuzi huo pia umeridhiwa na Rais Jakaya Kikwete.
Waziri Ghasia amesema kuwa Wakurugenzi wengine watatu wapewa onyo kali, ambao ni wa Rombo, Busege na Muheza na wengine watatu wakipewa onyo la kawaida, wakurugenzi hao ni wa Manispaa Ilala, Hai na Mvomero.