Yaya Jolly Tumuhirwe aliyekiri kosa hilo mahakamani baada ya kusema alimchapa mtoto kwa sababu naye alikuwa anachapwa na mama wa mtoto huyo.
Yaya wa huyo ambaye alinaswa kwa kanda ya video akimchapa na kumkanyaga mtoto mdogo amehukumiwa leo asubuhi na mahakama kwenda jera miaka minne kama adhabu ya kosa hilo.
Aidha awali Jolly Tumuhirwe aliambia mahakama kuwa alilazimika kufanya kitendo chake kwa sababu mamake mtoto huyo aliwahi kumchapa mara kadhaa.
Alipokuwa anaondoka kortini mama wa mtoto Angella Mbabazi, alikanausha madai ya Jolly akisema hajawahi kumgusa Jolly hata wakati mmoja.
Alihoji madai ya Jolly akisema angewezaje kumchapa msichana huyo wa kazi na kisha amuache na mtoto wake?
Awali tuhuma dhidi ya Jolly kuwa alimtesa mtoto huyo, yalitupiliwa mbali na mwendesha wa mashitaka wakisema ingekuwa vigumu ,kuweza kuyathibitisha