Manchester United wameibonda Liverpool Bao 3-0 Uwanjani Old Trafford na kuzoa ushindi wao wa 6 mfululizo kwenye Ligi Kuu Uingereza leo Desemba 14,2014, unaowabakisha Nafasi ya 3.
Man United walikwenda Haftaimu wakiwa Bao 2-0 mbele kwa Bao zilizofungwa na Wayne Rooney Dakika ya 12 na Juan Mata Dakika ya 40.

Kipindi cha Pili, Robin van Persie aliipa Man United Bao la 3 katika Dakika ya 71.
Ushindi huu umewafanya Man United wawe Pointi 8 nyuma ya Vinara Chelsea na Pointi 5 nyuma ya Timu ya Pili Man City.

Mechi inayofuata kwa Man United ni hapo Desemba 20 Ugenini huko Villa Park dhidi ya Aston Villa.




Hapo jana Desemba 13,2014,usiku,Bao 2 za Olivier Giroud na 2 za Santi Cazorla zimewapa Arsenal ushindi wa Bao 4-1 walipocheza kwao Emirates na Newcastle na kuwapandisha hadi Nafasi ya 6 wakiwa Pointi 2 nyuma ya Timu ya 4 West Ham na Timu ya 3 Manchester United.

Ushindi huu ulileta ahueni kwa Mashabiki wa Arsenal ambao baadhi yao walimshangilia Meneja wao Arsene Wenger baada ya Wiki iliyopita kufungwa na kumtaka Wenger ang’oke.



 
Top