Baadhi ya wakazi wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera wamelalamikia kutofika kwa vifaa vinavyohusika katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa hadi muda wa kufungwa kwa vituo vya kupigia kura
Baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo wameeleza kusikitishwa na kitendo cha kutopiga kura hadi muda wa kufungwa vituo ulipofika kwa kuwa wamepoteza haki yao ya msingi bila kuwa na taarifa yoyote
Kati ya maeneo yaliyokumbwa na tatizo hilo ni pamoja na kituo cha Nyalulama, Mubuhenge, Mukikomelo na Mwivuza ambako Masanduku pamoja na Karatasi za Kupigia kura hazijafika hadi kufikia muda wa kufungwa kwa vituo vya kupigia kura
Hata Hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Bw Cornel Ngudungi ambaye ndiye msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo wilayani Ngara akilitolea ufafanuzi changamoto hizo amesema ni vijiji 59 havijashiriki upigaji kura na kwamba vitafanya uchaguzi huo kesho kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni.
Awali Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Constantine Kanyasu amesema vifaa vimechelewa kufika kutokana na tatizo la magari ya kusafirisha vifaa hivyo
Habari Na:-Radio Kwizera FM-Ngara.