Jeshi la Polisi mkoani Kagera limefanikiwa kuwauwa majambazi sita waliokuwa wanapanga kuteka mabasi katika eneo la ngazi saba wilayani Biharamulo.
Akizungumza mkoani Kagera kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Henri Mwaibambe amesema jeshi la Polisi lilipata taarifa ya kwamba kunakundi la majambazi linafanya mpango wa kuteka magari na kufanya uporaji katika eneo la ngazi saba wilayani Biharamulo ambapo jeshi hilo lilifanya doria na kufanikiwa kuwauwa majambaizi sita. 

Kamanda Mwaibambe ameongeza kuwa kati ya majambazi hao sita ni mmoja tu aliyetambulika kwa jina Gahungu Gerad raia wa Burundi na wengine watano bado hawajafahamika.

Hata hivyo kamanda Mwaibambe ametoa onyo kwa wahalifu mbalimbali kwa kuwataka waache kabisa kufanya vitendo vya uhalifu kwani serikali inamkono mrefu wakiutawala na kwamba jeshi la Polisi sasa limeimarisha ulinzi katika mapori ya Kasindaga na Biharamulo kwa lengo la kudhibiti majambazi wanao ingia kutoka nchi jirani za Rwanda, Burundi na Uganda.

 
Top