Katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Maganga Sengerema akitoa heshima za mwisho kwa marehemu Daudi Lusalula Mbatiro(56) aliyekuwa katibu wa CCM kata ya Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga aliyeuawa juzi kwa kuchinjwa na watu wasiofahamika eneo la Malenge lililoko kati ya kata ya Kagongwa na Mwalugulu-picha na Mohab Dominic-Kahama
Awali waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa marehemu nyumbani kwake katika kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu wilayani Kahama ambapo mamia ya watu walijitokeza katika mazishi hayo yaliyohudhuriwa na viongozi wa siasa na serikali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga wakiongozwa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja-picha na Mohab Dominic-Kahama
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akiaga mwili wa marehemu jana Jumapili katika kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga-picha na Mohab Dominic-Kahama
Sanduku lililobeba mwili wa marehemu kabla ya mazishi-picha na Mohab Dominic-Kahama
Wa pili kutoka kushoto ni katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Maganga Sengerema akiwa na mwenyekiti wa CCM mkoa Khamis Mgeja(kulia kwake) wakiweka udongo kaburini-picha na Mohab Dominic-Kahama
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akizungumza baada ya mazishi ambapo alisema serikali na kamati ya ulinzi imejipanga vizuri kufuatilia tukio hilo na kuomba wananchi kuwa wavumilivu ni pigo kubwa kwa jamii na familia na ccm kwa kupoteza kiongozi wao-picha na Mohab Dominic-Kahama
Credit:Malunde1