Kikosi cha Kabanga Boys
Kwa mujibu wa reporters wa mtandao huu wa Ngara yetu, jana siku ya jumapili ya tarehe 7/12/2014 zimechezwa mechi za kirafiki za mpira wa miguu katika viwanja viwili tofauti. Mechi ya kwanza iliwakutanisha Murusagamba fc na Ngara Boys ambapo mchezo huo ulichezwa katika uwanja wa Murusangamba maarufu kama uwanja wa machinjioni. Katika mchezo huo timu zote mbili zilitoka sare ya kutokufungana hivyo wote kuondoka wababe uwanjani.
Kikosi cha Bodaboda fc
Mchezo wa pili uliwakutanisha Kabanga boys na Bodaboda fc zote za mji mdogo wa Kabanga, katika mchezo huo ulotazamwa na mamia ya mashabiki timu ya Kabanga Boys iliibuka na ushindi mnono wa gori 9 kwa 1 dhidi ya timu ya boda boda fc, hivyo mchezo ulimalizika kwa timu ya Kabanga boys kuibuka wababe.

Timu zikijiandaa kuingia uwanjani


Picha na Ezra Whatsapp no.0766378713

 
Top