Mbunge wa arumeru mashariki Joshua Nasari aliyekamatwa jana jioni leo tarehe 17/12/2014 amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya arumeru na kusomewa shitaka la kuharibu mali kwa kuchana bendera ya chama cha mapinduzi CCM katika kijiji cha EMBESERI na kuachiwa kwa dhamana.
Mbunge huyo alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa tano asubuhi na kusomewa shitaka la kuharibu mali kwa kuchana bendera ya CCM na hakimu wa mahakama ya wilaya ya meru David Mwita kuwa mnamo tarehe 16 mwezi Desemba mtuhumiwa alitenda kosa hilo katika kijiji cha EMBESERI ambapo mtuhumiwa alikana kosa na kuachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni moja na nusu pamoja na wadhamini watatu na kesi yake itatajwa tena tarehe 24 mwezi huu.

Baada ya kutoka mahamani akiwa nje ya mahakama mbunge huyo amesema anashangaa kupewa kesi hiyo kwa kosa ambalo hajawahi kutenda lakini hiyo inatokana na wivu wa kupata vitongoji vingi katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mara ya kwanza na atorudi nyuma kwa vitisho hivyo.

Naye mbunge wa arusha mjini Godbles Lema amesema fitina hizo zitafika mwisho kwani mashariti aliyowekewa mbunge huyo yanaonesha kuwa walitaka kumkomoa lakini chadema ipo imara na kamwe Haitarudi nyuma.

Chanzo: ITV

 
Top