Habari zilizopatikana kutoka mnada wa Tinde ulioko katika kata ya Tinde wilaya ya Shinyanga, ambao hufanyika kila siku ya Jumanne ni kwamba mwanamme mmoja ambaye jina lake halijafahamika mara moja anadaiwa kupasuliwa kichwa na wananchi waliokuwa eneo la mnada.
Mdau wa Malunde1 blog Paul De Nyoso Seseja aliyepo eneo la tukio anasema tukio hilo limetokea jioni hii ya tarehe 17/12/2014 na limetokana na mwanamme huyo kupamia/kuparamia fungu la vitunguu vilivyokuwa vinauzwa katika soko hilo kitendo ambacho kiliamsha hasira kwa watu waliokuwa eneo hilo baada ya mtuhumiwa aliyeonekana kulewa pombe kuonesha ubabe baada ya kuulizwa kwanini kapalamia vitunguu hivyo

Mwanamme huyo akiwa ameanguka chini baada ya kupigwa kwa fimbo na wananchi katika mnada wa Tinde ambapo inadaiwa kuwa amepasuka kichwa

Wasamaria wema wakitoa msaada kwa mwanamme huyo kabla ya kumkimbiza katika zahanati ya Tinde kwa ajili ya matibabu
Safari kuelekea zahanati ya Tinde.

Credit: Malunde 1



 
Top