Wasamalia waliokuwepo eneo la tukio wakisaidiana kumbeba mtu mmoja aliepoteza fahamu baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Vilio vilitawala wakazi wa nyumba hiyo baada ya kutokea kwa tukio hilo.
Sehemu ya mali zilizookolewa.
Nyumba moja mali ya mzee Nampembe, mkoani Lindi imeteketea kwa moto juzi usiku na kupelekea baadhi ya mali zilizokuwemo ndani ya nyumba hiyo kuteketea. Hali hiyo ilipekekea wananchi wa eneo la jirani na nyumba hiyo kupiga mawe gari la zimamoto baada ya kuchelewa kufika eneo la tukio kwa ajili ya kuzima moto huo.

Mmoja kati ya wakazi wa nyumba hiyo amepoteza fahamu baada ya kupatwa na mshituko. Chanzo cha moto huo kimeelezwa kuwa ni mshumaa baada ya kukosekana umeme mjini Lindi.

 
Top