Mkuu wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera,Bw. Lambris Kipuyo (katikati) akizindua boti ya Umoja wa Wavuvi wa kisiwa cha mazinga wilayani Muleba,Desemba 20,2014...Boti hiyo iendayo kwa mwendo kasi ina lengo la kuthibiti vitendo vya ujambazi ndani ya ziwa victoria na kuweza kulinda wavuvi pamoja na mali zao..Picha Na:-Shabani Ndyamukama-MULEBA.
Mkuu wa wilaya ya Muleba mkoani Kagera,Bw. Lambris Kipuyo akikata utepe kuzindua boti ya Umoja wa Wavuvi wa kisiwa cha mazinga wilayani humo,katika uzinduzi huo aliambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo huku akiwataka wananchi kuhakikisha wanashirikiana na vyombo vya dola kudhibiti wahalifu.
Aidha Mwakilishi wa Kamanda wa polisi mkoani Kagera Henry Mwaibambe ambaye alikuwa mkuu wa jeshi la polisi wilayani Muleba, Salvas Makweli amesema askari polisi watashirikiana na wananchi kufanya doria kila mara.
Makweli amesema askari hao hawana budi kufanya kwa kuzingatia maadili ya jeshi hilo na kushirikiana na wananchi kuwabaini wahalifu bila kuwanyanyasa wananchi na mali zao hatimaye kuwamisha mikakati ya kuwepo kwa boti hiyo.
Katika hatua nyingine diwani wa kata ya Mazinga Alex Thadeo amesema boti hiyo itatumia lita 600 kwa mwezi lakini bado wavuvi wanazo Sh 42 milioni na kuhitaji Sh 15milioni toka serikalini ili kununua boti itakayogharimu Sh 72 milioni .
“Wavuvi tumejiwekea malengo ya kuchangishana fedha kununua boti za doria baada ya kuathiriwa na majambazi ambao huwakata viungo vya mwili watumishi wetu na kuwanyang’anya mashine na zana za uvuvi”Alisema Thadeo
Wilaya ya Muleba yenye kilomita za mraba 10,737 inavyo vijiji 166 na kata 43 pamoja na visiwa 33 ambavyo vinakaliwa na watu wakifanya shughuli zao ni 26 ambapo katika mapato ya halmashauri asilimia 70 hutoka visiwani humo.