Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Geita Joseph Msukuma(PICHANI) amejikuta katika wakati mgumu baa ya kuzomewa kama mtoto na wananchi kutokana na kile kilichotajwa wananchi wamegundua kuwa mambo ambayo amekuwa akiwaambia na kuwaahidi ni ya uongo.
Hali hiyo imejitokeza jana mbele ya naibu waziri wa fedha nchini Mwigulu Nchemba kwenye mkutano wa hadhara kuzindua kampeni zao za uchaguzi serikali za mitaa, uliofanyika katika viwanja vya shule ya msingi Nyankumbu wilayani Geita Mkoani Geita.
Tukio hilo la aina yake lilitokea mara baada ya Msukuma kusimama na kuanza kuongea na wananchi kwa kuanza na salamu ya Chama,akisema CCM oyeeee!! wananchi wenye hasira waliokuwepo nao walianza kusema PEOPLES POWER!!.
Mbali na wananchi kuitikia kwa salamu ya CHADEMA pia walimtaka kushuka jukwaani na wengine wakisema mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Geita ni muongo hakuna ukweli anaousema kazi yake ni kuwaponda wenzake ndani ya nje ya CCM.
Mwenyekiti huyo alipoona hasikilizwi aliamua kuwaamuru greengurd kuanza kuwakamata wananchi wote waliokuwa hawamsikilizi na kuanza kukimbia ovyo hali iliyosababisha mkutano huo kusimama kwa takribani dakika 10.
“Kamateni wote ambao ni Wanachadema na muwalete hapa, kwanini wapige kelele wakati mimi naongea kama mwenyekiti wa Chama tawala "alisema Msukuma.
Baada ya vurugu hizo za kumtaka mwenyekiti huyo kushuka jukwani kuzidi askari wakutuliza ghasia FFU wakiwa na Gari lenye No.PT 1998 huku wakiwa na bunduki pamoja na mabomu walifika kutuliza vurugu hizo.
Askari hao walimkamata kijana mmoja ambaye hakutambulika jina lake mara moja na kumshushia kipigo kikali huku wakimtupia kwenye gari na kuondoka naye.
Baada ya vurugu kuisha,mwenyekiti huyo aliendelea kuhutubia huku akiwatupia lawama viongozi wa serikali kwa kudai kuwa viongozi ambao wanachumia matumbo yao hali iliyowafanya wananchi kuanza kuondoka mmoja mmoja.
Naye naibu waziri wakati wa hotuba yake alisema hawatakubili kuendelea kuwakumbatia viongozi wote ambao ni wezi hata kama wanatoka chama ch chake watashugulikiwa kwa mujibu wa sheria bila kujali ni nani.
Katika hatua nyingine mwandishi wa habari hizi alishuhudia magari zaidi ya matano yakisomba wananchi kutoka vijijini kuja kwenye mkutano yakiwemo malori na hiace lakini cha kushangaza mara baada ya mkutano kuisha baadhi ya wananchi walitelekezwa bila kurudishwa makwao.
Madereva walisikika wakisema"...Jamani tumepewa pesa ya kuwaleta kwenye mkutano hatukupewa pesa ya kuwarudisha, tafuteni viongozi wenu waweze kuwarudisha tulipowatoa, alisema dereva mmoja”.
Na Valence Robert-Malunde1 blog Geita