Diamond Platnumz ameingia Dar es salaam Tanzania leo Dec 02 akiwa na tuzo zake 3 alizozipata kutoka Channel O ambapo Watanzania wamejikusanya barabarani kutoka Airpot mpaka mitaa aliyokuwa amepita.
Msafara ulipotoka Airpot umepitia Buguruni mpaka Kariakoo ambapo ulipofika Kariakoo ilibidi Jeshi la Polisi liingilie kati ili kupunguza foleni ya watu waliokuwa wakitaka kumshika mkono Diamond.
Diamond alipofika Buguruni aliamua kushuka kwenye gari ya wazi aliyokuwa amepanda na kutembea kwa miguu na mashabiki wake mpaka Kariakoo,hizi ni baadhi ya picha za mapokezi yake hayo.

 
Top