Mchezaji wa zamani Arsenal na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Thierry Henry ametangaza kustaafu kucheza soka baada ya kucheza kwa miaka 20.
Mchezaji huyo ambaye akiwa na Ufaransa walichukua kombe la dunia mwaka 1998 na mwenye miaka 37 aliondoka kwenye timu ya New York Red Bulls mwezi huu.
Henry anajiunga na Sky Sports baada ya kuwa mchambuzi kwenye kombe la dunia kwenye kituo cha runinga cha BBC. Mchezaji huyo amewahi pia kuchezea Juventus, Barcelona na Monaco.

 
Top