Leo ni mwaka wa 53 tangu upatikane uhuru wa Tanzania bara(Tanganyika) kutoka kwa muingereza, kama ilivyo ada ya miaka mingi, 9 Desemba huwa kuna sherehe za kuadhimisha siku hii na leo ntajitahidi kuwaeleza kinachojiri uwanja wa Uhuru, Tuwe pamoja.
Sherehe zimeshaanza na sasa hivi mshehereshaji anatambulisha viongozi mbali mbali wa gwaride. Viongozi mbali mbali wa kitaifa na wageni waalikwa washafika ndani ya uwanja wa Uhuru. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Kikwete ndio anasubiriwa ili maadhimisho ya sherehe ya Muungano wa Tanzania uanze.

- Rais wa awamu ya pili mh. Ali Hassan Mwinyi ndio anaingia kwenye uwanja wa uhuru akiwa kaongozana na mke wake.

- Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idi anawasili kwenye eneo la tukio akiwa kaongozana na wake zake wawili.

- Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na rais wa Bunge la SADC anawasili kwenye uwanja wa tukio.

- Makamu wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mh. Seif Sharif Hamad anawasili

- Waziri mkuu wa JMT mh. Peter Kayanza Pinda anawasili kwenye uwanja wa Uhuru.

Anaesubiriwa sasa na raisi wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Mh Ali Shein, anaingia na kuelekea kwenye sehemu yake iliyotengwa baada ya kusalimiana na meza kuu.

Msemaji anaendelea kutambulisha uongozi wa gwaride leo

Anaewasili ni mke wa raisi, mama Salma Kikwete

Msemaji anatoa ratiba ya leo na raisi ataondoka viwanjani mishale ya saa sita baada ya maadhimisho

Raisi wa Jamhuri anaingia ndani ya uwanja wa uhuru na watu wanamshangilia sana hapa, anaenda kwenye jukwaa lilitengwa kusubiri wimbo wa taifa.

Rais anaelekea kukagua gwaride la vikosi vilivyopo hapa uwanjani, raisi anasalimiana na jukwaa kuu na kukaa kwenye kiti chake

Sasa gwaride linapita mbele ya rais.

 
Top