Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania,TFDA imefuta usajili wa aina tano za dawa baada ya kubaini kuwa zina madhara na hazifai kwa matumizi ya Binadamu. TFDA imefikia hatua hiyo baada ya dawa hizo kubainika kuwa na viambata vinavyosababisha maradhi sugu ikiwemo kiharusi, na wakati mwingine kusababisha vifo na kuamuru aina tano za dawa za binadamu ziondolewe sokoni na vituo vyote vya kutolea huduma za afya nchini kote mara moja .
Aina tano za dawa zinazotajwa kufutiwa usajili na kuzuia uingizwaji kuwa ni pamoja na dawa ya kutibu Fungus ya vidonge na Kasuli aina ya Ketoconazole, dawa ya kutibu Malaria ya maji na vidonge aina ya Amodiaquine (Monotherapy), dawa za kutibu mafua na kikohozi za maji, vidonge na Kapsuli zenye kiambato hai aina ya Phenylpropanlo Amine, dawa ya kuua bakteria ya sindano aina ya Chloramphenicol Sodium Succinate inayotengenezwa na kiwanda cha Lincoln Pharmaceuticals Ltd, India na dawa ya Kuua bakteria ya maji na kapsuli aina ya Cloxacillin.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Bw.Hiit Sillo amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya uchunguzi wa kitaalam wa muda mrefu kwa kutumia mifumo ya ufuatiliaji wa usalama na ubora wa dawa ambao pia unafanya kazi kwa kutumia mtandao wa kimataifa kwa ushirikiano wa shirika la afya duniani WHO.
Aidha TFDA imefanya mabadiliko ya matumizi ya dawa ya maralia ya SP kutumika kama kinga ya maralia kwa wanawake wajawazito tu na kuagiza watengenezaji kubadili machapisho na vifungashio vyake mara moja.
Mkurugenzi wa Dawa TFDA, Mitanga Fimbo, pamoja na kufafanua athari zake amewataka watoa huduma nchini kote kuondoa dawa hizo na kuziteketeza mara moja kabla ya kuanza kwa msako.