Pichani ni Wazee, Viongozi wa dini pamoja na wakuu wa Idara katika Halmashauri ya wilaya ya Ngara Mkoani Kagera wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Kagera Bw John Mongela akiongea nao wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kubaini changamoto zake wilayani Ngara Februari 02 na 03 ,2015.



Mkuu huyo wa Mkoa wa Kagera , Bw John Mongela (aliyesimama pichani) akitumia fursa ya kuongea na Wazee wa wilaya Ngara na aliwataka Wananchi wenye sifa mkoani Kagera kujitokeza kushiriki zoezi la kujiandikisha katika Daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kutumia haki yao ya Msingi ya Kupiga Kura kwenye uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu,2015.

Bw Mongela pia amezitaka Taasisi za dini kuepuka kampeni za Kisiasa katika nyumba za Ibada wakati wa kuelekea kuipigia Kura ya Maoni Katiba Inayopendekezwa na kusisitiza kuwa mijadala ya Kisiasa haipaswi kufanyika kwenye nyumba za ibada na wanaokubali ama kukataa kuipitisha katiba inayopendekezwa wanapaswa kwenda majukwani kueleza uzuri na ubaya wa Katiba hiyo na sio kwenye makanisa au misikiti.

 
Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw Costantine Kanyasu akiongea jambo wakati Mkuu wa mkoa wa Kagera Bw.Mongela alipozungumza na Wazee wa wilaya ya Ngara kwenye ukumbi wa Halmashauri.


Aidha pia Mkuu wa Mkoa wa Kagera ,amebainisha kuwa Serikali Mkoani Kagera, inatarajia kufanya Oparesheni dhidi ya watu wanaojihusisha na wizi wa mifugo katika kata ya Kasulo wilayani Ngara na kwamba ni hali ya kuchosha kusikia habari za wizi wa mifugo katika kata hiyo mara kwa mara, hivyo ni lazima hatua zichukuliwe ili kudhibiti vitendo hivyo.
 
Bw Mongela ametoa kauli hiyo kufuatia malalamiko ya baadhi ya wakazi wa kijiji hicho, waliodai kuwa kwa sasa wafugaji hawana amani kutokana na kukithiri kwa vitendo vya wizi wa mifugo huku wahusika wakiwa hawachukuliwi hatua zozote.
 
Akitembelea nyumba ya Masista wa Buhororo mjini Ngara, wakati akikagua miradi ya maji katika ziara yake ya siku 2, amewaagiza watendaji katika Halmashauri ya wilaya ya Ngara kuhakikisha wanapeleka huduma muhimu kwa wananchi muda wote badala ya kusubiri ziara za viongozi.

Amesema mara nyingi wananchi wamekuwa hawapati huduma muhimu ikiwemo maji lakini huduma hizo hupatikana pale viongozi wa juu wanapofanya ziara katika maeneo husika.


Bw Mongela akitembelea nyumba ya Masista wa Buhororo mjini Ngara, wakati akikagua miradi ya maji katika ziara yake ya siku 2, amewaagiza watendaji katika Halmashauri ya wilaya ya Ngara kuhakikisha wanapeleka huduma muhimu kwa wananchi muda wote badala ya kusubiri ziara za viongozi.

Amesema mara nyingi wananchi wamekuwa hawapati huduma muhimu ikiwemo maji lakini huduma hizo hupatikana pale viongozi wa juu wanapofanya ziara katika maeneo husika

Picha zote Na:-Shaaban Ndyamukama




 
 
Top