Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal akiweka shada la maua katika mojawapo ya makaburi ya wanafamilia.
Mojawapo ya jeneza likishushwa kaburini.

Ndugu wa marehemu wakilia kwa uchungu wakati wa mazishi.

Mmoja wa wanandugu akipewa huduma ya kwanza baada ya kuanguka wakati wa mazishi hayo.

MAKAMU wa Rais, Dk. Gharib Bilal leo amewaongoza mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam katika mazishi ya watu sita wa familia moja waliofariki dunia katika ajali ya moto iliyotokea wiki iliyopita huko Kipunguni jijini Dar es Salaam.

Mazishi hayo yamefanyika leo katika makaburi ya Airwing, Keko jijini Dar e s Salaam huku yakiuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa vyama na serikali, taasisi na makampuni binafsi.

Akizungumza kwa huzuni wakati akiwapa pole ndugu, majirani, marafiki pamoja na Watanzania wote kwa ujumla, Dk. Bilal amewataka Watanzaia kuwa na utaratibu wa kuwa na vifaa vya kuzimia moto katika kila nyumba na kuwa na ufahamu wa namba 114 ya Jeshi la Zima Moto ili kutoa taarifa mapema lakini pia kutengeneza madirisha na milango itakayoweza kusaidia kujiokoa wakati wa majanga kama hayo.

Wanafamilia hao walioteketea katika moto huo unaodaiwa kutokana na hitilafu ya umeme ni pamoja na David Mpira (60), Celina Yegela (50) (Dada wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya, Lucas Mpira (20), Celina Emmanuel (9), Pauline Emmanuel (4) na Samwel Yegela.
 
 
Top