Siku tatu tu baada ya watu watatu kuuawa kwa kukatwa mapanga kisha kufungiwa ndani ya nyumba zaidi ya siku 5 katika kijiji cha Bugogo wilaya ya Shinyanga,mauaji ya watu wa kukatwa mapanga yameendelea kujitokeza ambapo huko katika kijiji cha Manyada,kata ya Usanda wilaya ya Shinyanga mwanamke mmoja ameuawa kwa kukatwa mapanga akiwa amelala nyumbani kwake.Tukio hilo limetokea jana saa nane usiku ambapo chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha(pichani) amemtaja aliyeuawa kuwa ni Winifrida Simon(35) ambaye alivamiwa akiwa amelala ndani ya nyumba yake na watu wasiofahamika kisha kukatwa mapanga kichwani na shingoni.

Na Kadama Malunde-Shinyanga 
 
 
Top