
Polisi mkoani Dodoma wanamsaka mkazi wa Chang’ombe Juu, Tisi Malya kwa kumuua askari polisi kwakumcharanga mapanga wakati akijaribu kumuokoa mtoto wa miezi minane aliyekuwa anataka kuuawa namtu huyo.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime amemtaja askari aliyeuawa jana majira ya saa 5:00 asubuhi kuwa ni Joseph Swai.Akisimulia mkasa huo kwa waandishi wa habari, Kamanda Misime alisema kuwa askari huyo aliitikia mwito uliofika kwake wa kuwepo kwa dalili ya tendo la jinai nyumbani kwa mkazi mmoja wa Chang’ombe Juu katika Manispaa ya Dodoma.

"Askari aliamua kumwokoa mtoto huyo kwa kumrukia mtuhumiwa, lakini kwa bahatimbaya aliteleza na ndipo mtuhumiwa akamkata kichwani askari wetu," alisema Misime.Alisema pamoja na askari huyo kuanguka, mtuhumiwa aliendelea kumkatakata kwa panga huku mtendaji na kijana waliyekwenda naye eneo la tukio, wakikimbia huku wakipiga kelele za kuomba msaada.Alisema mtuhumiwa baada yakufanya kitendo hicho cha kinyama, alikimbia akiwa na panga lake huku nguo zake zikiwa zimetapakaa damu.
Aidha, alisema katika hekaheka hizo, mama wa mtoto baada ya kuona mtoto amebwagwa na askari ameanguka chini, naye alimkwapua mtoto na kukimbia naye mahali pasipojulikana. Alisema polisi wanamsaka baba huyo na mama huyo kwa ajili ya usalama wake..
Na Josephine Charles-Malunde1 blog Dodoma.