Mbunge wa Kigoma Kusini, David
Kafulila, ambaye ni Katibu
Mwenezi wa Chama cha NCCR-
Mageuzi, amesema hana sababu
yoyote ya kuhama chama chake
na kujiunga na chama kipya cha
siasa cha Alliance for Change and
Transparency (ACT-Tanzania).
Kafulila alisema hayo jana
alipokuwa akijibu swali kuhusu
kusambaa kwa tetesi katika
mitandao ya kijamii kwamba,
anahamia chama hicho
akiambatana na aliyekuwa
Mbunge wa Kigoma Kaskazini,
Zitto Kabwe aliyehamia chama
hicho hivi karibuni.
“Tetesi hizo zinatokana na tabia
yangu ya kuwa na marafiki wengi
katika chama hicho kipya, lakini
nashangaa nina marafiki wengi
CCM na hata Chadema, lakini
hawasemi nahamia vyama hivyo
ila ACT. Hizo ni tetesi tu sina
sababu ya kuhama chama
changu,” alisema.
Alisema Zitto alihama Chadema
kutokana na mgogoro uliokuwepo
baina yake na Chadema, hivyo
alikuwa na sababu ila yeye
akihama bila kuwa na sababu,
itakuwa haina maana.
Alisema yeye bado ni Katibu
Mwenezi wa NCCR-Mageuzi na
anaendelea na kampeni za
kujenga chama hicho ikiwemo
yeye kurudi bungeni pamoja na
chama hicho kuongeza wabunge
wengi zaidi.
Home
»
SIASA
» Kafulila Aikana
ACT Wazalendo
afunguka mengi
kuhusu yeye
kutaka kuhamia
ACT Wazalendo