Watu saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 48 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Msanga Line walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na basi la Luwinzo katika eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, wilaya Kilosa, Morogoro.
Ajali hiyo ilitokea juzi March 19,2015, saa 6:45 mchana, baada ya basi la Msanga Line linalosafiri Dar es Salaam kwenda Mahenge, wilayani Ulanga, Morogoro kugongana na basi la Luwinzo lililokuwa linatoka Njombe kwenda Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Leonard Poul (pichani), chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa madereva wa mabasi yote ambayo walishindwa kuyamudu.
Alisema majeruhi wengi wa ajali hiyo wamelazwa katika hospitali ya Mtakatifu Kizito wakisubiri utaratibu wa kupelekwa katika Mospitali ya mkoa wa Morogoro.
Inaelezwa kua watu sita walifariki dunia papo hapo na mwingine amefariki wakati akiwa njiani kupelekwa hospitalini kupata matibabu.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema hadi sasa mwili mmoja tu ndiyo uliotambulika na miili mingine sita bado haijatambulika na imehifadhiwa katika hospitali ya St Kizito Mikumi
Ajali hizi zimekuwa zikiongezeka kwa kasi hasa ikikumbukwa ni wiki iliyopita tu Taifa limetoka kuomboleza vifo vya watu 50 waliofariki kwenye ajali mkoani Iringa.
Licha ya Serikali kufanya juhudi bado ajali za mabasi kugongana na malori zinaendelea kuchukua roho za Wantanzia ambao bado walikuwa wanahitajika kwenye ujenzi wa Taifa.
Tumuombe Mwenyeezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema, peponi Ameni.