Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
Kundi hatari la vijana limeibuka
wilayani mwanga mkoani
Kilimanjaro na kuzua hofu. Kundi
hilo la vijana wapatao 40, wanadaiwa
kupewa mafunzo ya kijeshi na watu
wasiofamika wilayani humo.
Vijana hao kwa muda wa miezi
kadhaa inadaiwa wamekuwa
wakipewa mafunzo ya kijeshi katika
vijiji vya Lang’ata na Kirya kwa lengo
la kuandaliwa kufanya matukio ya
kihalifu nchini.
Habari za uhakika kutoka wilayani
Mwanga zinasema hali hiyo imezua
wasiwasi mkubwa kwa wananchi
ambao walipiga simu polisi kuomba
msaada.
Akizungumza na MTANZANIA jana,
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Shaibu
Ndemanga, alikiri kuwapo taarifa
hizo.
“Taarifa hizi nimezisikia tangu juzi,
tunazifanyia kazi, sina uhakika, sina
cha kusema kwa sasa.
“Tumesambaza askari karibu
maeneo yote hadi muda huu
tunaongea wapo doria wanaendelea
na msako mkali,” alisema Ndemanga.
Alisema polisi na vyombo vingine vya
dola wanafanya kazi usiku na
mchana ili kuhakikisha wananchi
wanakuwa salama.
“Nakuhakikishia ndugu yetu, askari
wetu wanafanya kazi usiku na
mchana, tunataka kuona wananchi
wanabaki salama na wanaendelea na
kazi zao kama kawaida,” alisema.
Alisema hadi jana wakazi wa eneo la
Lang’ata na Kirya wamekuwa
wakipiga simu polisi kuomba msaada
kutokana na uwepo wa kundi hilo la
vijana wanaopewa mafunzo
yanayodaiwa kuwa huenda
yanaweza kuwa chanzo cha kuibuka
kwa matukio ya kigaidi nchini.
“Wananchi wanapiga simu na
kutwambia kuna watu, lakini
mwenyewe nimekwenda hadi huko
sikufanikiwa… naomba uwe na
subira nitawajulisha maendeleo ya
msako huu,” alisema Ndemanga.
Habari zinasema eneo la Lang’ata
ambalo liko karibu na Bwawa la
Nyumba ya Mungu, limezungukwa
na pori ambalo linaweza kutumiwa
na wahalifu.
Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, Godfrey Kamwela,
alipoulizwa kuhusu tukio hilo,
alisema hana taarifa lakini akaomba
apewe muda wa kulifuatilia.
“Ndiyo nimesikia kwako, naomba
unipe muda kidogo nilifuatilie,
maana hatuwezi kupuuza taarifa
zinazotufikia,” alisema Kamanda
Kamwela.
Matukio ya vijana kupewa mafunzo
ya kijeshi na hata kudaiwa
kuandaliwa kwa ajili ya kufanya
vitendo vya kigaidi, yamekuwa
yakijitokeza kila wakati nchini.
Oktoba 7, mwaka 2013, Jeshi la Polisi
mkoani Mtwara liliwashikilia watu
11 kwa tuhuma za kupata mafunzo
ya kijeshi msituni kwa kutumia CDs
za al-Shabaab.
Tukio hilo la aina yake lilitokea
katika Mlima Makolionga, Wilaya ya
Nanyumbu mkoani humo ambapo
pia CDs zenye mafunzo v
8mbalimbali ya kijeshi 25
zilikamatwa.
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Mtwara, Zelothe Stephen, alisema
watuhumiwa hao
walikamatwa baada ya jeshi lake
kupata taarifa kutoka kwa
wasamaria wema.
“CD hizo zilikuwa zinatoa mafunzo
ya Al-Shabaab ya kuchinja watu,
mauaji ya Osama bin Laden,
Zindukeni Zanzibar, Kuandaa
Majeshi, Mauaji ya Idd Amin na
Mogadishu Sniper,” alisema Zolothe.
Alisema watuhumiwa wote ni wakazi
wa Wilaya ya Nanyumbu na kwamba
walikuwa wakiongozwa na Mohamed
Makande, 39, mkazi wa Kijiji cha
Sengenya ambaye pia alikamatwa.
Vitu walivyokamatwa navyo
watuhumiwa hao ni mapanga
mawili, deki ya DVD, solar, visu,
tochi, betri, simu za kiganjani 5,
vyombo mbalimbali vya kulia
chakula, baiskeli tatu, vitabu
mbalimbali vya dini ya Kiislamu,
unga wa mahindi kilo 50, mahindi
kilo 150 na virago vya kulalia.
Vingine ni mfuko wa kijani
unaosadikiwa ni wa kijeshi wenye
nembo ya nanga ya meli yenye
mistari kulia na kushoto na nyoka
katikati.
Chanzo: Mtanzania