Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Vedasto Kilosa mkazi wa Kabanga wilayani Ngara mkoani Kagera alikutwa amejinyonga wodini alikolazwa katika hospitali ya Murganzwa wilayani Ngara kwa kutumia shuka usiku wa kuamkia tarehe 14/04/2015.
Aidha ndugu wa marehemu waliiambia Ngara yetu kuwa kabla ya marehemu kuchukua uamuzi huo alifikishwa hospitalini hapo kwa tatizo la kuchanganyikiwa akili. Aidha baadhi ya jamaa zake wanasema marehemu alikuwa na tatizo hilo lililoanza mwezi Novemba mwaka jana japo lilikuwa likitulia kwa muda.
Marehemu atazikwa leo tarehe 15/04/2015 majira ya saa nane nyumbani kwake kabanga walayani Ngara.