Wanamgambo wa Al shabaab.Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Imesema kuwa ipo katika tahadhari dhidi ya uwezekano wa kushambuliwa kikundi cha ugaidi katika miji ya Dar es salaam na Mwanza.
Kwa mujibu wa waziri wa Mambo ya ndani Mathias Chikawe amesema kwamba nchi ipo katika tahadhari ya juu kufuatia taarifa za vyombo vya habari kuripoyi kwamba, kuna uwezekano wa shambulio la ugaidi katika miji ya Dar es salaam na Mwanza.
Hatua inafuatia baada ya taarifa zilizo bainisha kuwa mmoja ya waliokamatwa katika shambulio la chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya ni Mtanzania. Mpaka sasa serikali ya Tanzania haijaweza kudhibitisha ripoti zinzaoenea, kuhusu shambulio la ugaidi nchini humo.
Pamoja na hayo waziri Chikawe amesema kuwa serikali ya Tanzania, inafahamu kuwa mmoja ya watuhumiwa walikokamatwa huko Garissa Kenya ni Mtanzania. Amesema watawasiliana na polisi wa Kenya wakimaliza kumhoji mtuhumiwa huyo.
Kwa upande mwingine Tanzania imewahi kukumbwa na shambulio la ugaidi mwaka 1998 wakati mabomu yalilipuka katika balozi za Marekani, jijini Dar es salaam na Nairobi, Kenya na kusababisha vifo ya watu wengi.