Mkuu wa mkoa wa kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya amewaongoza mamia ya wakazi wa manispaa ya Kigoma Ujiji kuaga miili ya watu wanane wakiwemo wanafunzi sita wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kibirizi Mjini Kigoma wali fariki dunia jana baada ya kupigwa na radi kufuatia mvua iliyonyesha kwa takribani masaa matatu.
Majonzi yalitawala shughuli hiyo hasa baada ya miili hiyo kupokelewa katika viwanja vya shule ya msingi Kibirizi kabla ya ndugu kukabidhiwa tayari kwa maziko huku mwili wa Mwalim Elieza Mbwambo ukisafirishwa kwenda Moshi kwa maziko .

Akitoa salamu za rambirambi mkuu wa mkoa wa Kigoma Luten Kanal Mstaafu Issa Machibya amewataka wafiwa na wananchi kuchukulia tatizo hilo kama ni tukio la ajali ya kawaida na kwamba msiba huo ni mzito.

Kwa upande wao viongozi wa dini Sheikh Moshi Guoguo kutoka Bakwata na mchungaji Emmanuel Mtoi wa kanisa la KKKT wakitoa mawaidha katika msiba huo, 
wamewataka waumini wa dini mbalimbali kujiandaa kwa kuwa kila mwanadamu ataonja mauti kwa wakati wake na kwamba imani za kishirikina zisihusishwe katika msiba huo.

BONYEZA HAPA NA LIKE KUJIUNGA NA MTANDAO WETU
 
Top