Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati akilivunja Bunge mjini Dodoma jana Julai 09,2015. Kulia ni Spika wa Bunge Anne Makinda. Picha na Edwin Mjwahuzi.
Rais Jakaya Kikwete amelihutubia Bunge la 10 kwa mara ya mwisho, akijikita katika takwimu zinazoonyesha mafanikio ambayo Serikali ya Awamu ya Nne imeyapata tangu alipoingia Ikulu mwaka 2005, lakini akakiri kutofanikiwa kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Hali iliyokuwa mwaka 2010 wakati alipohutubia Bunge hilo kwa mara ya kwanza, ndiyo iliyojirudia jana Julai 09,2015, baada ya wabunge wa vyama vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia vikao na kuwaacha wapinzani wachache.

Rais Kikwete, ambaye alihutubia kwa saa 2.20 alitangaza kulivunja Bunge la 10 lakini akasema litavunjwa rasmi Agosti 20,2015, akieleza kuwa shughuli ya jana ilikuwa kama “kitchen party au send off”.

Katika hotuba yake, Rais Kikwete alimmwagia sifa Spika Anne Makinda, wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na viongozi mbalimbali wa Serikali, wananchi na chama chake kwa kumuamini, huku akisisitiza kuwa anaondoka madarakani na kuiacha nchi ikiwa salama.BOFYA HAPA KUSOMA - Hotuba ya Rais Kikwete Wakati wa Kuagana na Wabunge na Kulivunja Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 


 
Top