Baba Askofu Severin Niwemugizi na Dr Sengati kulia.

Wanachama watatu wa Chama cha Mapinduzi wilayani Ngara Mkoani Kagera wamechukua Fomu za Kuwania Ubunge wa Jimbo la Ngara ikiwa ni siku moja tangu kuanza kwa zoezi la kutoa Fomu za Ubunge na Udiwani.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi wilayani Ngara Bw Jacob Makuneamewataja waliochukua Fomu hizo kuwa ni Bw Cyprian Muheranyi, Bi Hellena Adrian Ghozi na Dr Philemon Sengati.

Akizungumza na Radio Kwizera Bw Cypriuan Muheranyi ambaye ni Mgombea wa kwanza kurudisha Fomu hiyo baada ya kuichukua hapo jana Julai 15,2015, ametoa wito kwa wakazi wa Ngara kujiepusha na vitendo vya Rushwa wakati wa Uchaguzi ili kupata viongozi bora watakaochochea Maendeleo.

Katibu wa CCM wilayani Ngara amesema zoezi la utoaji wa Fomu za Ubunge linakwenda pamoja na utoaji wa Fomu za Udiwani kwenye Ofisi za CCM katika Kata za wilaya hiyo ,likianza jana Julai 15 hadi Julai 19,2015 ambapo ametoa wito kwa Wanachama wenye sifa kujitokeza kuchukua Fomu hizo.

Source:-Radio Kwizera.
 
Top