- Mwanasoka bora wa Dunia, Lionel Messi amefunga mabao yote,wakati FC Barcelona ikiilaza 2-0 Arsenal katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jana February 23,2016 kwenye Uwanja wa Emirates,London.Messi amefunga mabao hayo dakika ya 71 akimalizia pasi ya Neymar wakati la pili alifunga kwa penalti dakika ya 83, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa na Mathieu Flamini.Arsenal sasa watalazimika kupanda mlima katika mchezo wa marudiano mwezi ujao Uwanja wa Camp Nou kwa kushinda 3-0 ili kwenda Robo Fainali.Katika mchezo mwingine,Juventus wakiwa nyumbani dhidi ya Buyern Munich, mchezo huo umemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kufuatia sare ya kufungana mabao 2-2.Bayern Munich ndio walioanza kuzigusa nyavu za wapinzani kwa kuandika bao la kuongoza kupitia kwa mchezaji wao Thomas Muller dakika ya 43, muda mchache baadaye Arjen Robben akaandika bao la pili kwa buyen Munich katika dakika ya 55 kipindi cha pili.Kwa upande wao Juventus walizinduka na kuandika bao la kwanza kupitia kwa Paulo Dybala ikiwa ni dakika ya 63 kipindi cha pili, huku Stefano Sturaro akiandika bao la pili la kusawazisha dakika ya 76 na kuufanya mchezo umalizike kwa sare ya kufungana bao 2-2.Bayern sasa wanaweza kusonga mbele hata kwa sare ya 0-0 au 1-1 katika mchezo wa marudiano Ujerumani, kwani watanufaika na sharia ya mabao ya ugenini.Michuano hiyo itaendelea tena Jumatano kwa Mechi 2 Dynamo Kiev ikiikaribisha Man City huko Ukraine na PSV Eindhoven wao watakuwa Wenyeji huko Uholanzi dhidi ya Atletico Madrid.
Home
»
MICHEZO
» KLABU BINGWA ULAYA 2015/2016:- Barcelona yaipa Arsenal … Bayern Munich na Juventus sare.