Wajeruhi wa ajali ya basi la abiria mali ya kampuni ya Simba mtoto lenye T 393 DDZ lililokuwa likitokea mkoani Tanga kwenda Dar es Salaam na kusababisha watu 11 kufariki na wengine 29 kujeruhiwa wamesema dreva wa gari lao alijitahidi kuwaokoa lakini dereva wa lori alikuwa akiwafuata.
Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Panga Mlima wilayani Korogwe mkoani Tanga, ikihusisha lori T 378 CFE lililokuwa limebeba malighafi inayotumika kwenye viwanda vya saruji likielekea jijini Tanga.
Walionusurika katika ajali hiyo wamesema dereva wao alijitahidi ipasavyo kulikwepa lori hilo lakini ikashindikana.
Hospitali ya Teule Muheza ndipo walipolazwa majeruji wa ajali hiyo,wakati wale wenye hali mbaya wanapelekwa hospitali ya mkoa kwa matibabu zaidi.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga,ACP Mihayo Msikhela amesema dereva wa lori alilala usinginzi kisha gari lake likafuata basi hilo.
Miili ya marehemu waliopatikana kwenye ajali hiyo imehifadhiwa katika hospitali ya Teule Muheza mkoani Tanga.