Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo wa Tanzania,Bw. Mwigulu Nchemba,Leo Jumanne,Februari 09,2016, ametembelea Kijiji cha Kigurukwa mkoani Morogoro kulikotokea mapigano ya Wakulima na Wafugaji yaliyosababisha kuuawa kwa mbuzi takribani 70.
Waziri Mwigulu ameagiza Kamati ya Ulinzi ya Mkoa kuhakikisha wote waliohusika katika tukio hilo wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Pia ameagiza kutekelezwa haraka hukumu ya Mahakama iliyotolewa mwaka 2005 iliyoagiza kuwekwa kwa mipaka kati ya eneo la wafugaji na wakulima.

Katika tukio hilo,Zaidi ya Mbuzi na kondoo 70 wamekatwa katwa na watu wanaodaiwa kuwa ni walinzi wa jadi kutoka Gairo wanaojulikana kwa jina la Mwanu '

Taarifa zinadai kuwa mifugo hiyo ilikula nusu ekari ya mazao ya mkulima mmoja kijijini hapo na taarifa zikawafikia walinzi hao ambao walifika na kukatakata mifugo hiyo mali ya mama mmoja mjane mfugaji wa jamii ya kimasai

Lakini Inadaiwa kuwa mifugo ya mama huyo haikuhusika kula mazao hayo bali ni mifugo ya mfugaji mwingine.


 
Top