Wafanyabiashara Wanne raia wa Tanzania wameuawa nchini Msumbiji watatu kati yao wakipigwa risasi baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi waliokuwa na silaha za moto na mapanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe, amesema wafanyabiashara hao wa Dhahabu walivamiwa wakiwa katika vibanda vyao vya kubadilishia fedha usiku wa Februari Nane mwaka huu na kisha kushambuliwa kwa risasi na mapanga ambapo baadhi yao walifariki papo hapo na wengine walifariki baada ya kufikishwa hospitalini.

Amesema kutokana na marehemu hao kuwa sio wakazi wa Mtwara, ilitolewa ruhusa ya kuisafirisha miili yao na baadhi ya ndugu na jamaa ambao waliipokea miili hiyo kwa ajili ya kuisafirisha mpaka sehemu husika kwa ajili ya shughuli za mazishi.

Kwa upande wa ndugu wa marehemu, Doto Ramadhani Mfanga, amesema marehemu hao walipigwa risasi na wawili kati yao walifariki papo hapo huku wawili wengine walifariki njiani wakati wakipelekwa hospitalini ambao ni Salumu Mfanga na Mariam Ramadhani.
 
Top