Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera,Bi Honoratha Chitandaakibadilishana Jimbo na Mbunge wa Jimbo la Ngara,Mhe.Alex Gashaza.
Na Shaaban Ndyamukama –NGARA. 

Watumishi watano wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera wamesimamishwa kazi kwa ajili ya uchunguzi wa ubadhilifu wa Sh15 milioni, zilizotolewa kwa ajili ya Sacos ya vijana na umoja wa bodaboda wilayani Ngara.

Mkuu wa wilaya ya Ngara, Bi.Honoratha Chitanda alisema hayo juzi kwenye kikao cha watumishi wakati wa kutoa tathmini ya ziara ya waziri mkuu wa Tanzania,Mhe Kasimu Majaliwa jana wilayani Ngara,Mkoani Kagera na kutekeleza maagizo yaliyotolewa kiutendaji.
Bi Chitanda aliwataja watumishi hao kuwa ni Helen Mkongwa ambaye ni Afisa Maendeleo ya jamii, Moses Chegele ,Mwenyekiti wa Vijana Ngara Saccos, Zera Ruben Mhasibu wa Ngara vijana Saccos na Mary Parangjo, mtia saini naCosmas Rubangula wa Idara ya Ardhi anahusika kuuza viwanja nyakati za usiku. 

Alisema wahusika hao wanafanya kazi idara ya maendeleo ya jamii kitengo cha vijana pia fedha hizo zilitolewa Januari Mwaka huu na kuingizwa benki akaunti ya Vijana Saccos, kisha kuondolewa kwa kila mmoja kuchukua kiwango chake.

Licha ya kusimamishwa kazi kwa uchunguzi, wametakiwa kutoa maelezo jeshi la polisi na kulipa fedha hizo ifikapo Machi 21 saa nne asubuhi, na kwamba Afisa ushirika wilayani humo Kurwa Ganashi anatakiwa kuwajibishwa kwa uzembe.
 
Top