Watu watano wamekufa na wengine tisa kujeruhiwa huku Naibu Waziri pamoja na Wabunge wa kamati ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakinusurika kifo baada ya msafara wao kugongana na Lori lililopoteza Mwelekeo.
Ajali hiyo iliyotokea leo March 21, 2016,Katika eneo la Mapinga wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani iliyohusisha magari manne yakiwemo mawili yaliyokuwa na Wabunge wa kamati ya Bunge ya TAMISEMI iliyokuwa ikikagua miradi iliyo chini yake.
Dereva wa gari ya Naibu Waziri ofisi ya Rais -TAMISEMI aitwaye Bw.Aziz Mgongolwa ambaye alikuwa na gari lililokuwa na Naibu Waziri Suleiman Jafoambalo lilikuwa la tatu na mawili ya mbele yake yaligongwa na kusababisha vifo na majeruhi.
Amesema, Ajali hiyo ilitokana na uzembe wa magari yaliyokuwa yakitokea Bagamoyo.
Waliofariki katika ajali hiyo ambao wametambuliwa mpaka sasa ni Hilda Msele (59), Mkuu wa Idara ya Mipango ya Uchumi, Makame Ally (40), Dereva wa Tasaf, Khalid Hassan (40), Tunsime Duncan, Mwanasheria wa Wilaya na Ludovick Palangya, Mchumi,wote hawa ni wafanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo.
Mara baada ya ajali hiyo na majeruhi kufikishwa hospitali ya wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya matibabu,Naibu Waziri Jafo alipiga simu kwa menejimenti ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kuagiza wajiandae kupokea majeruhi wa ajali hiyo kwa Hospitali hiyo ya wilaya ya Bagamoyo haina uwezo wa kuwatibu.
Majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Taifa ua Muhimbili ni Ibrahim Matovu, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bagamoyo, Juliana Msaghaa, Mhandisi wa Maji wilaya, Dorothy Njetile, Mratibu wa Tasaf, George Mashauri, Mweka Hazina wa Wilaya, Amadeus Mbuta, Mshauri wa Tasaf, Julius Mwanganda, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Tauliza Halidi, Mwananchi na Amari Mohamed, Mwananchi.
Aliyepelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na kuruhusiwa ni Grace Mbilinyi ambaye ni Afisa Utumishi na Utawala wa Wilaya.
Ajali hiyo ilihusisha lori la mchanga, gari dogo yaliyokuwa yanatokea Bagamoyo kuja Dar es Salaam, na magari mawili yaliyokuwa kwenye msafara wa Kamati hiyo.
Magari yaliyokuwa katika msafara wa kamati hiyo, ni gari la Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na gari la Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo ambayo yaligongwa na lori hilo la mchanga na kusababisha vifo vya watu hao na kuwajeruhi wengine kadhaa.Na ITV -TANZANIA.