Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Pichani ) amesema katika kipinda cha siku 128 za serikali ya awamu ya 5 kumefanyika mambo mengi ya mafanikio kwa taifa.

Akizungumza kwenye kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Kagera,Usiku huu wa leo March 15,2016, katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara,Mhe. Kassim Majaliwa amesema serikali inajitahidi kufanya kazi kuhakikisha serikali inakua na uwezo kifedha katika kutekeleza miradi ya wananchi.

Amesema ni wajibu wa kila Mtanzania kuwafichua wala rushwa, mafisadi na wanaokwepa kodi.

Katika ziara hiyo ya siku 3 mkoani Kagera, Waziri Mkuu , Mhe. Kassim Majaliwa amefanya mikutano 20, ameweka mawe ya msingi na kukagua miradi 7 ya maendeleo, mikutano ya ndani 6 na mikutano ya hadhara mitano huku akisimamishwa na wananchi mara 2 njiani.


Mkuu wa wilaya ya Ngara,mkoani Kagera Bi. Honoratha Chitanda akifatilia Hotuba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa wakati Akizungumza kwenye kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Kagera katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Ngara,usiku huu wa leo March 15, 2016.

Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo wa Tanzania,Mhe. Mwigulu Nchembaakiambatana na Waziri Mkuu katika Ziara hiyo ya siku 3 mkoani Kagera.

 
Top