Pichani wa pili kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania ,Dkt.Elia Kibwa akikata utepe kufungua Mahafali ya 6 ya Kidato cha Sita 2016 ya Shule ya Sekondari Kabanga ,wilayani Ngara mkoani Kagera  April 16, 2016.
Kulia ni Mkuu wa Shule hiyo Bw Aaron Dishon Sekazoya,na Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Bw.Julius Sendama na Kaimu Afisa Elimu Idara ya Sekondari wilayani Ngara Bw Gerald Muhile (kushoto.)

Wahitimu wa kidato cha sita katika shule ya sekondari kabanga wilayani Ngara Mkoani Kagera, wameitaka serikali kuboresha elimu nchini kwa kweka miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika shule za msingi sekondari 

Wamebainisha hayo  April 16, 2016, katika mahafali ya sita ya shule hiyo kwa kidato cha sita na kwamba katika shule nyingi hapa nchini zinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa , matundu ya vyoo, madawati, vitabu vya kiada na ziada pamoja na uhaba wa maktaba zenye viwango katika utoaji wa taaluma ya elimu.

Wahitimu hao 147 wa kidato cha sita kati yao wasichana ni 46 na wavulana ni 101 walio katika mchepuo wa masomo ya CBG na HKL huku shule yote kuanzia kidato cha kwanza hadi cha tano jumla yao ni wanafunzi 869 kati yao wasichana ni 388.


Mkuu wa Shule ya Sekondari Kabanga ,Bw. Aaron Dishon Sekazoya akitoa taarifa ya Maendeleo na Changamoto mbalimbali katika Shule yake wakati wa Mahafali ya 6 ya Kidato cha Sita 2016 Shule ya Sekondari Kabanga ,wilayani Ngara mkoani Kagera  April 16, 2016.

Wanafunzi wa shule hiyo wamesema wanakabiliwa na changamoto ya malazi kwa kukosa mabweni kwani wanatumia vyumba vya madarasa na kulala wanafunzi wawili katika kitanda kimoja kwa kuwa vitanda ni pungufu

“Licha ya kupata chakula hapa shuleni tunapanga foleni kutafuta huduma ya choo na wengine tunachafua mazingira tukijisaidia vichakani jambo ambalo tunahofia kukumbwa na magonjwa ya mlipuko” Alisema mmoja wa Wanafunzi wa shule hiyo.

Aidha shule hiyo haina bwalo na wanafunzi kulia chakula chini ya miti huku wakikosa maktaba, vitabu vya masomo ya Sayansi, walimu wa masomo hayo pamoja na kukatika kwa umeme na maji na kuwakatisha tamaa katika taaluma.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania ,Dkt.Elia Kibwa akikabidhi Cheti kwa mmoja wa Mhitimu wa Kidato cha Sita wakati wa Mahafali ya 6 ya Kidato cha Sita 2016 ya Shule ya Sekondari Kabanga ,wilayani Ngara mkoani Kagera jana April 16, 2016.


Mkuu wa shule hiyo Bw.Aaron Dishon Sekazoya ( Pichani ) amesema jitihada zilizofanywa na shule hiyo ni kukarabati madawati 150 na vitanda 46 kwa thamani ya Sh150 000 na kwamba kanisa la Anglikan wilayani Ngara kupitiaTumaini Fund utajenga matundu 10 ya vyoo kwa thamani ya Sh40 milioni.

Bw.Sekazoya amesema changamoto zilizotajwa za kukosa bwalo na ukumbi wa mikutano ni pamoja na uhaba wa Hostel, kwani iliyopo ni moja yenye kutosheleza wanafunzi 90 tu na mabweni yapo mawili na kuhitajika mabweni matatu.

Amesema shule hiyo inahitaji vitanda 200 vya wanafunzi vilivyopo 174 vinavyotumiwa na wanafunzi 87 walioko katika hostel tatu nab ado mahitaji ni nyingine tatu zenye kutumiwa na wanafunzi 240

Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dr Elia Kibwa ambaye ni mkazi wa wilaya ya Ngara ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo , amesema walimu waandae mazingira ya wanafunzi kwa kupanda miti ambayo itawasaidia kupata zana za kufundishia

Aidha amesema akiwa ndiye mwalimu wa kwanza katika shule hiyo mwaka 1990 ndoto zake ni wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi sita kujengwa kisaikolojia kuingia katika Chuo Kikuu kwa kuwa na ujuzi kupitia masomo ya Sayansi.

“Ndoto zangu nahitaji watakaomaliza kidato cha sita hapa waingie Chuo kikuu katika wilaya yetu ili wazawa wapate wageni kutoka wilaya na mikoa mingine na kujifunza mila na tamaduni za makabila mbalimbali” Alisema Dr Elia Kibwa.

Katika hatua nyingine amesisitiza walimu kuwafundisha wanafunzi masomo ya Sayansi , Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHAMA ili kuingia katika ushindani wa kimawasiliano katika kujifunza wakitumia mitandao na kompyuta

HABARI/PICHA Na:-Shaaban Ndyamukama-Ngara/Kagera.
 
Top