Uwanja wa Kabanga ulitumika kuupokea Mwenge wa uhuru uliokesha uwanjani hapo tarehe 23/07/2016 lakini mpaka sasa uwanja huo bado mabaki ya vibanda hivyo hayajaondolewa ili kupisha michezo kuendelea katika uwanja huo.
Wadau wa michezo wameiomba kamati ya mwenge wilaya ya Ngara kushughulikia suala hilo la kuondoa vibanda hivyo au kutoa ruksa ya kuondoa vibanda hivyo ili kupisha michezo kuendelea uwanjani hapo ikiwemo ligi ya mpira wa miguu inayoendelea uwanjani hapo.