Mashemasi 16 walioko Kanisa la Anglikan wilayani Ngara katika Dayosisi ya Kagera wamepata daraja la uchungaji baada ya kuhitimu mafunzo ya biblia na misingi ya kanisa Hilo katika Vyuo mbalimbali hapa nchini.
Askofu wa Kanisa la Anglikan wilayani ngara Dr Aaron Kijanjali amewapatia daraja hilo leo, July 24, 2016 katika kanisa kuu la Murugwanza wilayani humo na amewataka kufanya kazi ya uchungaji kwa uadilifu na uaminifu kutangaza injili ya Mungu.
Dr Kijanjali amesema wachungaji hao wakumbuke wametumia rasilimali za familia na kanisa wakati wakiwa masomoni hivyo wailinde heshima yao pamoja na kanisa wakitegemea kuongozwa na taratibu, kanuni na sheria za kanisa.
Amesema licha ya kuwa wachungaji wanapaswa kudumisha upendo ngazi ya familia na waamini wao wakati wakijiandaa kuingia kwenye daraja la kuitwa kasisi nafasi ambayo inahitaji ufunguo kutoka kwenye mamlaka ya Mungu.
Pichani WACHUNGAJI NA MAKANONI WAMEWAWEKEA MIKONO WAKIONGOZWA MASHEMASI , Wakiongozwa na Askofu Dr Aaron Kijanjali katika ibada maalum iliyofanyika kanisa Kuu la Murugwanza mjini Ngara Mkoani Kagera.