Rais John Magufuli , leo anatarajiwa kuzindua ukuta wa machimbo ya madini ya Tanzanite,iliopo eneo la Mererani, kaskazini mwa nchini Tanzania
Ukuta huo wenye urefu wa kilomita 24.5 na urefu wa mita tatu kwenda juu, umejengwa kufuatia agizo lililotolewa na Rais John Magufuli, kama jitihada za kudhibiti na kuzuia utoroshwaji wa madini hayo, ambayo yanapatikana nchini Tanzania pekee.
Machimbo ya madini ya Tanzanite yazungushwa ukuta
Rais Magufuli ameagiza kujengwa ukuta kuzunguka mgodi wa Tanzanite Mirerani
Awali, Mwezi Februari, wakuu wa vyombo vya usalama, walitembelea eneo hilo, kuukagua ukuta huo uliojengwa kwa gharama za Kitanzania isiyozidi bilioni 6.
Walisisitiza kuwa lengo la kujengwa kwake ni kuzuia uhalifu na si kuwazuia wachimbaji wakubwa na wadogo kupata riziki zao.
Wakitoa taarifa kwa viongozi wa ulinzi, wataalamu waliojenga ukuta huo, walisema licha ya kufanikisha ujenzi huo, changamoto mbalimbali walikutana nazo ikiwemo hatari inayo ukabili ukuta huo, kutokana na wachimbaji kulipua baruti, karibu na ukuta, hivyo kusababisha hatari za kuharibika haraka.
Ugumu wengine walioupata ni uchimbaji katika maeneo yenye miamba.