Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara Mkoani Kagera, Bw.Aidan Bahama (kulia) akimuamulu kumwaga Pombe yake mmoja wa mwananchi aliyekutwa akinywa pombe katika kijiji cha Ngundusi kata ya Kabanga wilayani humo April 5,2018 huku sheria ikiwataka kunywa na Wafanyabiashara ya Pombe kufanya biashara yao baada ya saa za kazi.
Unywaji wa pombe za kienyeji ambao wakati mwingine huambatana na baadhi ya wanywaji kufanya vurugu, ukatili wa kijinsia, uporaji na hata kujeruhi.
Maafisa Watendaji wa Vijiji na Kata wakiweno Wenyeviti wa Vijiji wilayani Ngara mkoani Kagera wameagizwa kukomesha uuzaji na utumiaji wa pombe saa za kazi vinginevyo watakaokamatwa watachukuliwa hatua za kinidhamu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya NgaraBw.Aidan Bahama ametoa agizo hilo April 5, 2018 akiwa katika kijiji cha Ngundusi kata ya Kabanga wilayani humo baada ya kuwakuta wananchi wamelewa saa za kazi.
Bw.Bahama amesema baadhi ya watumiaji wa pombe katika vijiji na mitaa ni viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia sheria lakini hawatimizi wajibu wao na kusababisha kuwama miradi ya maendeleo na watu kuwa maskini.
"Kupitia kwa wananchi hawa niliowakuta wanalewa asubuhi hii naagiza vijii vyote atakayekutwa akiywa pombe saa za kazi akamatwe maana hao ndio wanachagia kuwepo kwa umaskini" AmesemaBw.Bahama.
Maagizo hayo ameyatoa baada ya kitembelea kijiji cha Ngundusi kata ya Kabanga akielekea kitongoji cha Mukitamo kusalimia Familia ya Mtoto Anthony aliyemzuia Baba yake asiuze shamba licha ya familia kuwa maskini kwa kukosa chakula na mahitaji mengine.
Hata hivyo Afisa Mtendaji wa Kata ya Kabanga wilayani NgaraVeronica Marthony amesema suala la ulevi saa za kati ni tatizo katika vijiji akiahidi kutekeleza maagizo ya Mkurugenzi kwa kuwachukulia hatua watakaohusiaka.
Picha/Habari Shaban Ndyamukama