MAJAMBAZI WASIOJULIKANA WAMEVAMIA NA KUVUNJA DUKA LA MATHAYO LUDOVICK MAARUFU KAMA BABA MAJA MKAZI WA KABANGA NGARA USIKU WA KUAMKIA TAREHE 28 MWEZI MEI 2014 NA KUPORA FEDHA AMBAZO THAMANI YAKE HAIJAJURIKANA, SIMU NA VITU VINGINE VINGI VILIVYOKUWEMO DUKANI HUMO.
AIDHA
MASHUHUDA WALIOKUWA WANAPITA NJIANI WAMESEMA WAHARIFU HAO WALIFANYA KITENDO
HICHO MAJIRA YA SAA SITA USIKU, AMBAPO KWA UOGA WAO WALIOGOPA KUPIGA KELELE YA
KUOMBA MSAADA WAKIDHANIA MAJAMBAZI HAO WANA SILAHA NZITO KAMA BUNDUKI MAANA
ZIMEZOELEKA KUTUMIKA KWENYE MATUKIO YA WIZI HASA MAENEO YA MIPAKANI.
MWENYE
DUKA NDUGU MATAYO AMESEMA WIZI HUO UMETOKEA NA PIA MLINZI WA DUKA HILO AMEKUWA
MZEMBE WA KUOMBA MSAADA MPAKA WEZI HAO WAMEVUNJA KUFURI ZA MILANGO NA KUINGIA NDANI YA DUKA HILO BILA
MLINZI KUCHUKUA HATUA YOYOTE YA KUOMBA MSAADA.
IMEZOELEKA
WALINZI WALIO WENGI MAENEO YA KABANGA HUWA WANAKUJA KAZINI WAMELEWA POMBE ZA
KIENYEJI HUSUSA NI GONGO HIVYO HUSINZIA NA KUSAHAU KAZI YAO YA ULINZI.
IKUMBUKWE
KUWA WIZI KAMA HUO ULIFANYIKA MWAKA JUZI KATIKA DUKA HILO AMBAPO WEZI WALIMUUA
MLINZI KWA KUMCHOMA KISU BAADA YA KUMKUTA AMELALA FOFOFO.
WANANCHI
WA KABANGA MUNAOMBWA KUDUMISHA ULINZI PIA NA KUTOKUWA WAOGA KWA KUSHRIKIANA NA
POLISI NAAMINI HAO WALIOWAONA WAKIVUNJA WWANGETOA TAARIFA POLISI WEZI HAO
WANGEKAMATWA.