Taarifa zilizotufikia hivi punde ni kwamba msanii maarufu katika uwanja wa tasnia ya filamu nchini Rachel Haule maarufu kama ‘Recho” amefariki dunia asubuhi ya leo hii.
Mauti hayo yamemkuta msanii huyo baada ya kujifungua kwa operation. Kutokana na hali yake kuto ridhisha ilibidi alazwe katika wodi ya ICU. Hata hivyo kwa bahati mbaya mauti yamemkuta asubuhi hii.
Msanii huyo ambaye amejinyakulia umaarufu nchini katika uwanja huu wa filamu, alikuwa ni miongoni mwa wasanii wenye mvuto kutokana na umbo lake pamoja na sura yake. Mavazi yake yaliyokuwa mafupi yalizidi kumfanya aonekane mrembo na mwenye mvuto kiasi cha kuwafanya watu wengi kutamani kufunga naye ndoa kwa hayohayo mavazi yake.