Taifa stars leo huko Harare , imefanikiwa kutoka sare ya bao 2-2 na Zimbabwe katika mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya mtoano ya AFCON 2015 na hivyo kufuzu kusonga raundi ya tatu ya mtoano kwa jumla ya magori 3 kwa 2 ambapo mechi ya kwanza iliyochezwa Dar es salaam Taifa stars ilishinda kwa gori 1 kwa 0.
Zimbwabwe walianza kufunga dakika ya 24, kabla ya Stars kusawazisha dakika kadhaa baadae kupitia Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 28.
Muda mchache baadae Thomas Ulimwengu aliongezea
Tanzania bao la pili dakika ya 46, kabla ya dakika 10 baadae Zimbwabwe
kusawazisha na kufanya matokeo 2-2.