Pichani ni jamaa/mwanamme ambaye hakujulikana jina wala makazi yake aliyenusurika kufa kutokana na kipigo cha wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kukuktwa akifanya jaribio la kutaka kumbaka mtot o mwenye umri wa miaka mitano jioni ya leo eneo la kata ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga.Tukio hili linakuja siku moja tu baada ya mazishi ya mtoto Happiness Kashinje mwenye umri wa miaka 9 kubakwa,kutobolewa macho kisha kuuawa na watu wasiojulikana katika kata jirani ya tukio la leo ya Ndala

Inaelezwa kuwa Jamaa huyu kakamatwa na wananchi mida ya saa 11,jioni lakini mpaka saa moja usiku alikuwa bado anapewa kipigo na wananchi hao,hadi pale jeshi la polisi lilipofika kuokoa maisha yake

Walioshuhudia tukio hilo wanasema Jamaa huyu kakutwa akimchezea sehemu za siri mtoto nje ya nyumba karibu na choo,na kufuatia kelele za mtoto huyo ndipo ndipo wasamaria wema wakaanza kumpa kipigo jamaa huyo


Mawe fimbo n.k,Wananchi wenye hasira wakiwa katika harakati za kumwadhibu jamaa huku viongozi wa mtaa na sungusungu wakizuia asipigwe


Ni katika eneo la tukio



Umati wa wananchi wakiwa eneo la tukio



Mmoja kati hawa watoto wawili kanusurika kufanyiwa unyama na jamaa aliyepigwa na wananchi wenye hasira jioni hii mjini Shinyanga(Jina la mtoto linahifadhiwa na Malunde1 blog kwa sababu za kimaadili)



Wananchi wakiwa na hasira


Viongozi wakizuia jamaa anayedaiwa kutaka kubaka mtoto asipigwe kwani wananchi walitaka kumchoma moto



Pichani ni jamaa/mwanamme ambaye hakujulikana jina wala makazi yake aliyenusurika kufa kutokana na kipigo cha wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kukuktwa akifanya jaribio la kutaka kumbaka mtot o mwenye umri wa miaka mitano jioni ya leo eneo la kata ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga

Baada ya jeshi la polisi kufika

Baada ya askari polisi kufika eneo la tukio,jamaa anapelekwa kwenye gari la polisi





Tayari kapanda kwenye gari la polisi,usiku huu



Polisi wanaondoka na mtuhumiwa wa ubakaji

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
 
Top