Vinara wa La Liga, Real Madrid, Jana Februari 14,2015 Usiku wakiwa kwao Santiago Bernabeu waliongeza pengo la uongozi wao na kuwa Pointi 4 mbele ya Timu ya Pili Barcelona baada ya kuwafunga Deportivo La Coruna Bao 2-0. Hadi Mapumziko Real waliongoza kwa Bao la Dakika ya 22 la Isco aliefunga baada ya Krosi ya Garreth Bale kumkuta Karim Benzema alieisindikiza Golini na Ronaldo kushindwa kuunganisha na Mpira kumkuta pembeni Arbeloa ambae aliurudisha nyuma na Isco kuachia Shuti lililotinga Wavuni.

Bao la Pili la Real Madrid lilifungwa Dakika ya 73 na Karim Benzema.
Nyota wa Real, Ronaldo na Garreth Bale, walikosa Mabao wakati Mashuti yao mawili yalipopiga Posti.


Hii Leo Jumapili Februari 15,2015 ,FC Barcelona watakuwa Nyumbani Nou Camp kucheza na Levante na Mabingwa Watetezi Atletico Madrid, ambao wako Pointi 7 nyuma ya Real Madrid , wako Ugenini kucheza na Celta Vigo.

LA LIGA 2014/2015 RATIBA/MATOKEO.

Ijumaa Februari 13,2015.

UD Almeria 2 Real Sociedad 2

Jumamosi Februari 14,2015.

Sevilla FC 3 Cordoba CF 0

Real Madrid CF 2 Deportivo La Coruna 0

Granada CF 0 Athletic de Bilbao 0

Malaga CF 0 RCD Espanyol 2

Jumapili Februari 15,2015.

1400Valencia C.F v Getafe CF

1900 FC Barcelona v Levante

2100 Rayo Vallecano v Villarreal CF

2300 Celta de Vigo v Atletico de Madrid

Jumatatu Februari 16,2015.

2245 SD Eibar v Elche CF 
 
 
Top